Paulinho ashukuru mashabiki kumkubali

Muktasari:

 Hivi sasa mchezaji huyo ameanza kukubalika na mashabiki wa Barca pamoja na wengine wa timu mbalimbali.

KIUNGO mpya wa Barcelona, Paulinho amewashukuru mashabiki wa klabu yake kwa kumkubali kikosini hapo kutokana na hapo awali uhamisho wake kutoka nchini China kukosolewa vikali.
 Hivi sasa mchezaji huyo ameanza kukubalika na mashabiki wa Barca pamoja na wengine wa timu mbalimbali.
Paulinho ameanza kuchomoa makucha yake kikosini hapo akishirikiana vema na staa wa timu hiyo, Lionel Messi na sasa ameshukuru kwamba mashabiki wa timu hiyo wameanza kumkubali kwa kasi tofauti na ilivyokuwa katika siku za nyuma.