Messi aionya Barcelona

Muktasari:

Staa huyo wa Italia alichemsha katika mechi mbili dhidi ya Real Madrid za Ligi ya Mabingwa Ulaya na inadaiwa Messi ambaye ana ushawishi mkubwa klabuni hapo, amewaambia mabosi wake waachane na mpango wa kumchukua Veratti.

INADAIWA kuwa staa wa Barcelona, Lionel Messi, amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba hamhitaji kiungo wa PSG, Marco Veratti, anayesakwa na Barcelona tangu dirisha kubwa lililopita la majira ya joto.