Mbappe ashawishiwa kutua Liverpool

Muktasari:

Fabinho amehama Monaco kwenda kujiunga na wakali hao wa Merseyside kwa ada ya Pauni 40 milioni mapema kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya moto wa Liverpool katika kunasa mastaa wa maana ambapo hadi sasa imeshawaweka kikosini wakali Naby Keita, Xherdan Shaqiri na kipa wa Kibrazili, Alisson Becker.

LIVERPOOL, ENGLAND. STAA mpya wa Liverpool, Fabinho amefichua kwamba amekuwa akimshawishi chinichini staa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ili atue huko Anfield wapige kazi.
Fabinho amehama Monaco kwenda kujiunga na wakali hao wa Merseyside kwa ada ya Pauni 40 milioni mapema kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya moto wa Liverpool katika kunasa mastaa wa maana ambapo hadi sasa imeshawaweka kikosini wakali Naby Keita, Xherdan Shaqiri na kipa wa Kibrazili, Alisson Becker.
Fabinho alisema kwamba amekuwa akitumia muda wake kumshawishi mchezaji mwenzake wa zamani wa Monaco, Mbappe kuhamia Liverpool kwa sababu wamekuwa wakizungumza na alimpongeza kwa uhamisho huo.
"Kylian alitumia meseji kunipongeza kwa kuhamia Liverpool," alisema Fabinho na kuongeza.
"Bado sijapata nafasi ya kumpongeza kwa kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia. Walichofanya Ufaransa kiliwa safi na alichofanya Mbappe kwa miaka miwili ya karibuni babkubwa. Anahitaji pongezi kubwa na nitafanya hivyo kumpongeza. Ameshasema kwamba msimu ujao atabaki PSG, lakini taratibu namshawishi aje Liverpool."
Mbappe alichaguliwa kuwa mchezaji bora kijana kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 na alikuwa kinda wa pili kufunga bao kwenye mechi ya fainali baada ya gwiji Pele.