Manchester City yainyonga Liverpool mabao 5-0

Saturday September 9 2017

 

London England. Timu ya Manchester City imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 baada ya kuifumua bila huruma Liverpool mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa leo Jumamosi.
Mabao ya Liverpool yamewekwa kimiani na wachezaji Sergio Aguero (1), Gabriel Jesus (2) na Leroy Sane ikiwa ni kipigo kikubwa kutolewa na klabu hiyo kwenye msimu huu mpya.
Kipigo hicho kimewaacha mdogo wazi vijana wa Jurgen Klopp ambao mpaka refa anapuliza filimbi ya mwisho walishika viuno wasiamini kilichotokea.