Leicester City wajisikilizia mkiani EPL

Muktasari:

Timu hiyo inanolewa na kocha Craig Shakespeare aliyerithi mikoba kutoka kwa kocha Claudio Ranieri aliyetimuliwa mwanzoni mwa msimu uliopita.

England. West Brom wamewaweka nafasi ngumu Leicester City katika nafasi ya tatu kutoka mwisho baada ya kutoa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England jana Jumatatu.
Msimu huu umeendelea kuwa kaa la moto kwa Leicester City ambao walikuwa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2015/16, ambapo hali haitofautiani sana na msimu uliopita ambao walipoteza mapema matumaini ya kutetea ubingwa wao.
Bao la Riyad Mahrez liliwatofanya kufuata aibu ya kufungwa nymbani ikiwa ni bao la kusawazisha.
Tangu kocha Craig Shakespeare achukue mikoba kikosini hapo, vijana wa Leicester City wameendelea kupambana lakini wakipata mafanikio kiduchu.