Rooney atapotezwa asipojiangalia

Tuesday October 10 2017

 

London, England. Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amemtaja nahodha wa timu ya taifa ya England, Harry Kane atakuwa bora zaidi ya Wayne Rooney.
Wright aliyewahi kuwa kinara wa mabao Arsenal na England, alisema Kane anaweza kuvunja rekodi ya Rooney katika kupachika mipira wavuni.
Pia alisema kuwa kocha Gareth Southgate, alikuwa sahihi kumpa majukumu ya kuingoza England katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Mshambuliaji huyo wa timu ya Tottenham Hotspurs, alifunga mabao mawili katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Slovenia na Lithunia. England ilishinda bao 1-0 katika kila mchezo.
Wright alisema hatashangaa mchezaji huyo endapo atavunja rekodi ya Rooney kwa kuwa ana kipaji cha kufunga na straika hodari.
"Tangu mwanzo nilisema Harry ni mchezaji hodari. Amejengewa msingi mzuri hakuna mtu wa kupinga uwezo wake uwanjani," alisema mchambuzi huyo wa soka England.
Mshambuliaji huyo amefikisha mabao 12 katika mechi 23 za timu ya taifa alizocheza na ameingia katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia.