Hawyard sasa rasmi kuivaa Philadelphia 76ers

Muktasari:

  • Hayward alizungumza na vyombo vya habari wiki hii na kueleza matarajio yake ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Philadelphia 76ers, huku akiweka wazi ana usongo na wa kufanya makubwa akiwa na jezi ya kijani ya timu yake hiyo.

NIMERUDI. Ndivyo anavyosema nyota na fowadi matata wa mabingwa wa kihistoria wa ligi ya NBA, Boston Celtics, Gordon Hayward baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kwa msimu mzima.

Hayward alizungumza na vyombo vya habari wiki hii na kueleza matarajio yake ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Philadelphia 76ers, huku akiweka wazi ana usongo na wa kufanya makubwa akiwa na jezi ya kijani ya timu yake hiyo.

Nyota huyo ambaye aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa ufunguzi msimu uliopita, amesema kwa sasa anarejea akiwa timamu kwa asilimia 100 baada ya kuwa nje akiishuhudia timu yake ikifika fainali ya Ukanda wa Mashariki na kuzuiliwa na

Clevaland Cavaliers.

Wakati kambi ya Celtics ikitarajiwa kuanza Septemba 24, kocha wa timu hiyo, Brad Stevens alisema kurejea kwa nyota huyo na wengine akiwemo Kyrie Irving, kutaongeza kitu na kuufanya msimu kuwa rahisi wakiwa tena na matarajio ya kucheza fainali msimu huu.