Jose Mourinho kumsajili Griezmann

Muktasari:

Griezmann, 26, amekuwa akisakwa na Man United kwa muda mrefu lakini klabu ya Atletico Madrid imekuwa ikimbania, lakini sasa kocha, Jose Mourinho, ameamua kuvaa magwanda na kuingia vitani kuhakikisha anamsajili mchezaji huyo.

MANCHESTER, England. Manchester United inahangaika kumnasa Antoine Griezmann lakini mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakijiuliza, mchezaji huyo atakapofika katika klabu hiyo, nani atakosa nafasi?
Taarifa ni kwamba, Henrikh Mkhitaryan ndio atakuwa katika wakati mgumu.
Griezmann, 26, amekuwa akisakwa na Man United kwa muda mrefu lakini klabu ya Atletico Madrid imekuwa ikimbania, lakini sasa kocha, Jose Mourinho, ameamua kuvaa magwanda na kuingia vitani kuhakikisha anamsajili mchezaji huyo.

Gazeti la L’Equipe lilisema kuwa Griezmann ataingia kwa kishindo katika kikosi cha kwanza.
Mkhitary analianza vizuri katika msimu huu huku akichangia upatikanaji wa mabao matano lakini katika siku za karibuni amekuwa akisuasua.
Hatahivyo Man United itakuwa na kazi ngumu ya kumnasa mchezaji huyo kwa kuwa ameongeza mkataba wake ambapo sasa utamalizika 2022.