Conte aambiwa Morata siyo mnyama kama Costa

Muktasari:

Costa na Conte kwa sasa hawana uhusiano mzuri tangu kocha huyo Mtaliano alipomtumia meseji straika wake huyo wa Kihispaniola akikwambia kwamba kwa msimu huu hana shida na huduma yake.

ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Chelsea, Ray Wilkins amemwambia Antonio Conte kwamba straika Alvaro Morata hawezi kumpa kitu cha uhakika kama ambacho angekipata kutoka kwa Diego Costa.
Costa na Conte kwa sasa hawana uhusiano mzuri tangu kocha huyo Mtaliano alipomtumia meseji straika wake huyo wa Kihispaniola akikwambia kwamba kwa msimu huu hana shida na huduma yake.
Kwa msimu uliopita, Costa alifunga mabao 24 kwenye Ligi Kuu England na kuifanya Chelsea kushinda ubingwa wa ligi hiyo, lakini Conte amemtimua fowadi huyo na kwenda kumsajili Morata kutoka Real Madrid.
Costa aliamini kwamba angeachana na Chelsea moja kwa moja na kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid, lakini dili hilo limekwama na sasa yupo kwao Brazil akiponda raha tu. Lakini, kocha Wilkins amemwambia Conte, Morata siyo mnyama kama Costa.