UEFA yatoa kikosi cha karne

Muktasari:

Kikosi hicho kina wachezaji sita kutoka klabu hizo za Hispania, nyota hao ni sita kutoka Barcelona na wanne wa Real wa sasa na zamani wa klabu hizo.

Madrid, Hispania. Real Madrid na Barcelona zimetawala soka la Ulaya katika miaka ya karibuni na UEFA wathibisha hilo kwa kuwajumuisha nyota wengi wa miamba hiyo ya Hispania katika kikosi cha wachezaji bora wa karne.
Kikosi hicho kina wachezaji sita kutoka klabu hizo za Hispania, nyota hao ni sita kutoka Barcelona na wanne wa Real wa sasa na zamani wa klabu hizo.
Katika kikosi kinaundwa na XI: Iker Casillas, Sergio Ramos, Gerard Pique, Carles Puyol, Philipp Lahm, Xavi, Andres Iniesta, Steven Gerrard, Thierry Henry, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Mshambuliaji Mreno amekuwa katika kikosi hicho cha UEFA kwa miaka 11, huku Messi amechaguliwa mara nane wakifuatiwa na Casillas, Puyol, Sergio Ramos na Iniesta (kila moja ameingia mara sita).