Baada ya miaka saba Arsenal yaifunga Spurs

Muktasari:

Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Shkodran Mustafi dakika 36 kabla ya Alexis Sanchez kuipatia Gunners bao la pili lililowapa pointi tatu na kuwafanya kuwa mbele kwa pointi moja kwa mahasimu zao hao.

London, England. Mabao ya Shkodran Mustafi na Alexis Sanchez yameifanya Arsenal kupata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Spurs tangu Machi, 2014, huku wenyeji wakitawala London derby kwenye Uwanja wa Emirates.
Bao la kwanza la Arsenal lilifungwa na Shkodran Mustafi dakika 36 kabla ya Alexis Sanchez kuipatia Gunners bao la pili lililowapa pointi tatu na kuwafanya kuwa mbele kwa pointi moja kwa mahasimu zao hao.
Spurs walipata nafasi nzuri ya kupata bao kupitia kiungo wake Christian Eriksen lakini shuti lake lilidakwa na kipa Petr Cech.
Mshambuliaji wa Spurs,Harry Kane alioneka bado hayupo fiti alipoteza nafasi nyingine ya kufunga bao akiwa katika eneo la hatari.
Kane pamoja na kiungo Dele Alli alikosa mechi mbili  za kirafiki za timu ya taifa ya England kutokana na kuumia walilazi kutolewa nje dakika 15 kabla ya filimbi ya mwisho na walipokuwa wakitoka nje walishangiliwa na mashabiki wa Arsenal waliojazana kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsene Wenger na Arsenal wamepanda hadi nafasi ya tano wakiwazidi kwa pointi moja vijana wa Mauricio Pochettino.