Willy Pozee ajishaua hadi aibu

Muktasari:

Baada ya kupeana hela laivu kwenye NTV ikiwa ni baada ya kuvua soksi ili kuvionyeshga viatu vyake vya Gucci, alipoitia mahojiano, siku chache baadaye alifanya kituko hata zaidi alipokwenda Citizen TV kwa mahojiano vile vile.

WILLY Paul au Pozee kwa hakika humwezi katika kutengeneza skendo. Wiki hizi amekuwa akikashifiwa sana kwa ujeuri wake na maringo ya kupitiliza.
Baada ya kupeana hela laivu kwenye NTV ikiwa ni baada ya kuvua soksi ili kuvionyeshga viatu vyake vya Gucci, alipoitia mahojiano, siku chache baadaye alifanya kituko hata zaidi alipokwenda Citizen TV kwa mahojiano vile vile.

Huko alitoa noti ya Sh 1000 na kujipanguzia jasho kwa kisingizio kuwa alikuwa kasahahu kubeba kitambaa. Kisha akampa shabiki wa kike noti hiyo.
Mahojiano pia yaliyokuwa yanakwenda kumalizika, alichomoa bunda la noti za 1000 na kuzitupa hewani na kuwaacha vijana ambao, hupamba shoo hiyo wakiziparamia.
Kitendo hicho kiliwakera mashabiki wengi waliokesha mitandaoni wakimkashifu kwa kupenda kujishaua na kuwa na maringo kupita kiasi wakati akidai yeye ni Mkristo safi.
Lakini, akizungumzia kitendo chake hicho, Willy kama kawaida alikana kuwahi kujishasha au kuringa bali alichokifanya ni kugawa kidogo alichonacho kwa mashabiki wake.
“Wajua wakati mwingine ni vizuri kuwagawia wenzako kile ulichobarikiwa na Mungu kwa sababu zote ni mali za dunia na tutaziacha hapa. So ukipata mgawie na ndugu yako ila kama pia kugawa ni maringo basi ni sawa,” jomba  akajikingia.