Straika wa Harambee Stars apigwa vijembe kwa kukosa chapaa!

Wednesday October 11 2017

 

By Na Vincent Opiyo

Kumekuwa na maneno mitaani kumhusu aliyekuwa straika wa Harambee Stars, Dennis Oliech kufilisika na kuishi maisha ya kufedhehesha licha ya kutengeza fedha wakati wake.
Oliech (32) alisacheza soka nchini Qatar, Ufaransa na Dubai akila mamilioni ya chapaa. Alicheza Kombe la Klabu Bingwa Ulaya akiwa Auxerre alipofunga magoli 25 kwenye mechi 165.
Wakati mmoja alilazimishwa kumshughUlikia mama yake Mary Oliech aliyekuwa akiigua saratani.
Inasemekana Oliech alitumia takribani Kshs. 123 milioni muda huo wote akirejesha afya ya mama yake. Ni jukumu si kila mtu anaweza kuchangamkia kwenye uchumi wa sasa lakini hivi karibuni Wakenya walianza kumkashifu kufuatia picha iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikiashiria kufilisika na kuishi maisha ya tabu.
Kiungo wa Harambee Stars, Johanna Omollo anayekipiga Cercle Brugge ya Ubelgiji amewakaomba Wakenya kuacha kumzungumzia vibaya jamaa ambaye goli lake dhidi ya Cape Verde liliipeleka Kenya fainali za kombe la mataifa bingwa barani mwaka 2004 nchini Tunisia.
“Oliech ni mmoja wa wachezaji bora ambaye tumemtazama akifanya makeke yake uwanjani. Ni gwiji  na anafaa kuheshimiwa. Ndio watu watazungumza kuhusu maisha yake haswa wakati anapitia changamoto za kawaida lakini hilo halibadilishi  mazuri aliyolifanyia taifa,” Omollo (28) alimweleza mwandishi kutoka mjini Brugge.