Cheki sifa za utamu wa Huddah

Muktasari:

Kwenye zile chokoza chokoza za safu hii kuhusu maisha yake hasa ya kimapenzi na ndoa, Soshiolaiti huyo mrembo ambaye siku hizi kazamia sana biashara za mitindo zaidi ya zile tabia zake za awali za kutupia picha za uchi kusaka kiki na kuuza sura, kadai kuwa hataki kabisa kuolewa.

SOSHIOLAITI maarufu nchini Huddah Monroe, ambaye siku za hivi karibuni kaonekana kutulia sana kwa kujitenga na utata, kaamka tena na jipya na kutrend kinoma noma.
Kwenye zile chokoza chokoza za safu hii kuhusu maisha yake hasa ya kimapenzi na ndoa, Soshiolaiti huyo mrembo ambaye siku hizi kazamia sana biashara za mitindo zaidi ya zile tabia zake za awali za kutupia picha za uchi kusaka kiki na kuuza sura, kadai kuwa hataki kabisa kuolewa.
Na ikiwa kwa bahati mbaya atampata mume wa kumuoa, basi asiwe Mnigeria ambao wameonekana kufurika jijini Nairobi na wengi kuyageuza makao yao.
Kuhusu ni kwa nini hawapendi wanaume wa Kinigeria, kichuna huyo mrembo alisema, “Wajua kila mtu ana testi yake na kwangu mwanzo siwezi kupenda kuolewa kabisa.
Na kama kwa bahati mbaya itokee hivyo, basi wakunioa walahi tena hatakuwa dume la Kinaija. Majamaa wanapenda ugomvi sana kuwapiga wanawake kila wakati halafu isitoshe hawajatulia wanapenda mademu wengi kupita maelezo.