Ai! Rayvanny na Bahati kumbe iko hivi

Muktasari:

Baada ya Bahati kuachia ‘Nikumbushe’ aliyomshirikisha mkali wa WCB, Rayvanny wiki iliyopita aliachia kete nyingine ‘Barua kwa mama’ na msanii wa densi kutoka Uganda, Eddy Kenzo.

HUKU wadau wakiendelea kumkashifu mwimbaji wa injili Bahati kwa kupotea njia baada yake kuonekana siku za hivi karibuni akiachia kolabo na wasanii wa muziki wa densi, mmoja wao kajitokeza kumkingia kifua.
Baada ya Bahati kuachia ‘Nikumbushe’ aliyomshirikisha mkali wa WCB, Rayvanny wiki iliyopita aliachia kete nyingine ‘Barua kwa mama’ na msanii wa densi kutoka Uganda, Eddy Kenzo.
Mtindo wake huu mpya unaoonekana kuasi injili umezidi kuibua mjadala mkali kuhusu haswa nyendo zake katika injili na kumsababishia wadau kumchana chana kwa kupoteza dira.
Lakini huku kashfa hizo zikiendelea, katokea mmoja wa wasani densi aliofanya kazi nao, Rayvanny ambaye kamkingia akisema wazo la kufanya na Bahati kazi lilikuwa ni lake.
“Mpango ulikuwa nije kufanya kazi na Khaligraph Jones kwanza, lakini Bahati ni mtu ninayemkubali sana na nilzipenda kazi zake. So nikawa naongea na bosi Tale (Meneja Babu Tale) kwamba nikipata nafasi ya kufanya kazi na Bahati itakuwa vizuri.
Lakini kabla sijamfikia nikiwa Kenya naye akanicheki akataka tufanye kazi. Nikamwambia kwa sababu unafanya injili basi wimbo tunaofanya usiwe wa kihuni ila inspirational na ndio akaja na wazo la Nikumbushe,” Rayvvany akamkingia. Msanii huyo wa Bongo amekuwa nchini kwa siku kadhaa kushiriki kwenye Coke Studio Season 5.