Drogba amkumbuka Tiote kwa bao

Muktasari:

Katika mechi hiyo, Drogba ambaye ni mmiliki mwenza wa klabu hiyo ya Phoenix, ambapo alikuwa nahodha alisaidia kushinda mabao 2-1 dhidi ya Whitecaps FC II, kisha akasema bao lake ni kwa ajili ya Tiote aliyefariki dunia akiwa anafanya kitu ambacho wote wanakipenda.

NEW YOK, MAREKANI. DIDIER Drogba na uzee wake aliifungia bao Phoenix Rising katika mechi yake ya kwanza kuichezea timu hiyo, kisha akasema bao hilo ni maalumu kwa staa mwenzake wa zamani wa Ivory Costa, Cheick Tiote, aliyefariki dunia Jumatatu iliyopita.
Katika mechi hiyo, Drogba ambaye ni mmiliki mwenza wa klabu hiyo ya Phoenix, ambapo alikuwa nahodha alisaidia kushinda mabao 2-1 dhidi ya Whitecaps FC II, kisha akasema bao lake ni kwa ajili ya Tiote aliyefariki dunia akiwa anafanya kitu ambacho wote wanakipenda. Tiote alifariki baada ya kuanguka uwanjani akiwa mazoezini kwenye klabu yake ya Beijing Enterprises.