Zlatan azindua game yake mpya

Muktasari:

  • Game hilo maudhui yake itakuwa ni kupigana litaanza kupatikana Agosti 17, imetengenezwa na kampuni ya kiswide ya ISBT GAMES imechukua takribani miaka miwili kukamilika na itaanza kupatikana katika simu za mkononi kupitia mfumo wa IOS na kufuatiwa na mfumo wa simu za Android.

Mshambuliaji mkongwe wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amezindua mchezo (game) yake mpya itwaayo Zlatan Legends

Game hilo maudhui yake itakuwa ni kupigana litaanza kupatikana Agosti 17, imetengenezwa na kampuni ya kiswide ya ISBT GAMES imechukua takribani miaka miwili kukamilika na itaanza kupatikana katika simu za mkononi kupitia mfumo wa IOS na kufuatiwa na mfumo wa simu za Android.

Katika video fupi ya tangazo la mchezo huo inasikika sauti ya ibrahimovic akisema “ Nilidhani hapatakua na changamoto zilizobakia. Ndivyo walivyokuja, mchezo mpya, sheria mpya na mpinzani mpya. Mtu ninae mjua vizuri. Katika siku hii ulimwengu utajua kwamba kuna Zlatan mmoja tu”

Baada ya maneno hayo anaonyeshwa mtu mwenye taswira kama ya Ibrahimovic akiwa amevaa mavazi ya suti za mapigano huku ametanua mikono yake kwa namna ile ile inayotumiwa na mchezaji huyo anaposhangilia pindi anapofunga goli.

Kwa sasa mchezaji huyo hana timu anayoichezea baada ya kufanyiwa oparesheni ya mguu kutokana na kuumia wakati akiitumikia Manchester  United, lakini kuna taarifa zinazosema huenda akaongezewa mkataba na timu hiyo.

Watu wanaisubiri kwa hamu game hilo ambapo bado haijafahamika kama itapatikana bure au kwa kulipia.