Zanzibar Heroes yaifungia kazi Kili Stars

Wednesday December 6 2017

 

By Vicent Opiyo

Kenya. Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes wameendelea na mazoezi katika Uwanja wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Machakos jioni ya leo Jumatano kwa ajili ya mechi kali dhidi ya majirani Kilimanjaro Stars Kombe la Chalenji hapo kesho Alhamisi.
Kikosi kipo chini ya mwalimu Hemed Suleiman mechi ya kesho itaanza saa mbili usiku, muda sawa na wanaofanya mazoezi.
Mechi hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ubora wa kila kikosi pamoja na kutoka eneo moja la Tanzania.