Yanga kujipima na Rhino Jumatano

Muktasari:

  • Yanga ipo katika harakati za kuvuna pointi zote kanda ya Ziwa msimu huu.

Tabora: Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga imewasili mkoani Tabora kwa ajili ya kambi pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki  na Rhino Rangers Jumatano.

Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United ya Shinyanga utakaopigwa Mkoani humo imepiga kambi hapa mkoani Tabora.

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema wameamua kutafuta mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni mpango wake wa kutaka kuwajaribu wachezaji wake.

Lwandamina alisema mbali na jaribio hilo pia anataka kuutumia mchezo huo kuwapa nafasi wachezaji wake waliokosa mchezo wa Kagera Sugar ambao timu yake ilishinda kwa mabao 2-1.

"Nikweli tumekubaliana tucheze hiyo mechi nafikiri itakuwa ni mechi nzuri itakayotoa kipimo kwa timu zote mbili,tutakuwa hapa kwa siku tatu ni vyema tukawapa kipimo wachezaji wetu,"alisema Lwandamina.