VIDEO: Yanga ya Moro yaiva mdogomdogo

Morogoro.Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema mpaka sasa wako tayari kwa Ligi Kuu baada ya mazoezi makali yanayoendelea mkoani Morogoro.

Beki Abdul amesema ratiba ya kufanya mazoezi mara mbili kwa siku imewapa nafasi nzuri ya kuiva haraka kabla ya kuanza ligi.

Nahodha huyo amesema wanajua ligi msimu ujao itakuwa ngumu, lakini malengo yao ni kuhakikisha wanaanzia na kumaliza wakiwa vinara.

Kaimu Afisa Habari wa Yanga, Godlisten Anderson amesema tangu wamefika Moro hakuna majeruhi yoyote katika kikosi chao.

Anderson amesema makipa wao wawili Benno Kakolanya na Ramadhan Kambwili wamechelewa kujiunga na  kambini kutokana na sababu mbalimbali.

Kakolanya hakuwepoo kambini kufuatia kufiwa na kaka yake ingawa amesharejea jana wakati Kabwili naye alikuwa na hudhuru.