VIDEO: Utambulisho wa Chilunda hapo CD Tenerifa kama Ronaldo

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa Azam, amesaini mkataba wa mkopo wa miaka mwili CD Tenerife na mchana huu atafanya mazoezi yake ya kwanza kwenye kituo cha Ciudad Deportiva Javier Perez.

Tenerife, Hispania. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Shabaan Idd Chilunda ametambulishwa rasmi leo katika klabu yake mpya ya CD Tenerife katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi Hatusa (Red Volkswagen Canarias).

Mshambuliaji huyo wa Azam, amesaini mkataba wa mkopo wa miaka mwili CD Tenerife na mchana huu atafanya mazoezi yake ya kwanza kwenye kituo cha Ciudad Deportiva Javier Perez.

Akizungumza mbele ya wanahabari, Chilunda alisema ni faraja kwangu kuwa hapa.

“Nilikuwa mwenye furaha kubwa tangu niliposikia CD Tenerife wananitaka nijiunge nao," alisema  Chilunda.

"Nipo katika kiwango kizuri, mazoezi yatakuwa tofauti na yale niliyokuwa nafanya nyumbani Tanzania, lakini haitokuwa vigumu kwangu kuzoea kwa sababu nipo tayari kwa maisha mapya."

"Mimi ni mshambuliaji sipo hapa kwa ajili ya kufunga tu, nipo hapa kwa ajili ya kushirikiana na wenzangu, nitasaidia kutegeneza nafasi za kufunga na kila kitu kinatakachokuwa ninaelekezwa kufanya."

"Nitajitoa kwa ajili ya wenzangu naamini haitachukua muda kuzoea hapa na kufanya kile ninachoelekezwa na kocha wangu."

"Nitacheza kwa nguvu na kwa kiwango kizuri, hilo siyo tatizo kwangu, japokuwa najua Hispania itakuwa tofauti, ila nitazoea kwa haraka."

"Faridi (Mussa) ni mfano mzuri kwangu, ninavyomuana nacheza sasa ni tofauti ilivyokuwa kabla," alisema Chilunda.

Mkurungezi wa ufundi wa CD Tenerife, Alfonso Serrano alisema Chilunda yupo hapo kwa mkopo wa miaka miwili akionyesha kiwango cha juu basi watamnunua moja kwa moja.

“Tunaimani na kiwango chake na rekodi yake ataanza kucheza katika mechi ya Agosti 17 na tutamuangalia jinsi anavyozoea hapa hadi Desemba."

"Chilunda hakuja hapa kufanya majaribio, tutachukua uamuzi juu yake kadri muda unavyokwenda, wawakilishi wake wametupa muda mrefu wa kukaa naye, alitakiwa kuwa hapa mapema ila urasimu umemchelewesha" alisema Serrano.

"Tunaimani naye, lakini hatutompa presha ya kuzoea hapa haraka tunaamini baada ya muda atakuwa sawa. Ni mwepesi anauwezo mkubwa wa kufunga mabao," alisema Serrano.