VIDEO: Rooney atua Washington, akaribia kuihama Everton

Washington.Wayne Rooney ametua Washington, Marekani kwa ajili ya kukamilisha mazingumzo na kufanya vipimo leo Alhamisi kuhusu uhamisho wake kutoka Everton kwenda DC United.
Jana, Rooney alikatisha mapumziko mafupi aliyokuwa pamoja na familia yake ndani ya Barbados ili kukamilisha mpango wake huo wa baadaye.
Rooney alikuwa katika Visiwa vya Caribbean tangu wiki iliyopita. Kwa sasa atakuwa akizungumzia kiasi cha Pauni 300,000 kwa wiki kutoka katika klabu hiyo mpango huo ukikamilika leo.

Uhamisho wa Rooney unatajwa kuwa wa Paundi 3.75 milioni kwa mwaka mmoja. Pia mpangop huo ukikamilika anatarajiwa kufanya vipimo vya afya yake,
Taarifa zaidi ilieeleza kuwa atafanya mazungumzo  na Mkurugenzi wa  DC United, Jason Levien pamoja pamoja na Kocha, Dave Kasper na atapata muda wa kutembea ndani ya  jiji hilo pamoja na kuutazama uwanja wao mpya wa Audi Field.