VIDEO: Manji habari nyingine, azua tafrani mkutanoni

MKUTANO wa klabu ya Yanga ulijikuta umemalizika ghafla baada ya wanachama kushindwa kuafikiana juu ya aliyekuwa mwenyekiti wao Yusuph Manji kujiuzulu.
Wakati mkutano ukiendelea, muendesha shughuli (MC), aliwauliza wanachama kwamba wanagapi wanaafiki mwenyekiti huyo kujiuzulu ndipo sakata likaibuka.
Wanachama walisikika wakisema hawaafiki Manji kujiuzulu lakini kuanza kupindisha pindisha kwa muendesha shughuli, wanachama waliona kama amewasaliti.
Wanachama walionekana kufura hasira kuona kama wanaondolewa mtu wao (Manji), kwani ghafla wote walinyayuka na kuanza kutoka kabla hata mkutano haujamalizika.
Hata hivyo katika mkutano huo, Yanga wamefanikiwa kutengeneza kamati maalum ya  kushughulikia usajili na mikataba yote ya wachezaji. Kamati hiyo imeundwa na wafuatao
 Abas Tarimba (mwenyekiti)
Mecky Sadik (makamu)
Wajumbe ni:
Abdallah bin Kleib
Nyika Hussein
Samuel Lukumay
Mashauri Lucas
Yusuphed Mhandeni
Ahmed Islam
Makaga Yanga
Ridhiwani Kikwete
Majid Suleiman
Hussein Ndama