Masawe ajipanga upya ya Ndanda FC

Muktasari:

  • Mchezaji huyo amejiunga na Ndanda msimu huu akitokea Stand United

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Ndanda FC, Jacob Masawe ameelezea maisha mapya ndani ya kikosi hicho kuwa ni tofauti na ilivyokuwa Stand United 'Chama la Wana'

Kabla ya kujiunga na Ndanda FC, Masawe alikuwa akichezea Stand United kwa zaidi ya miaka sita tangu ikiwa Ligi Daraja la Kwanza, jambo analosema walimzoea kujua ubora wake na mapungufu yake.

"Kila timu ina mipango yake na jinsi inavyoendesha maisha ya wachezaji wao  najitahidi kuzoea changamoto ya mazingira hususani mimi siyo muongeaji sana, hivyo lazima waanze kunizoea kihivyo kwanza ndipo watajua mimi ni wa aina gani," alisema.

Anataja kinachomsaidia kutojiana mpweke kuwa ni  kujuana na wachezaji aliyokuwa anakutana nao kwenye ligi na sasa wapo pamoja.

"Kinachosaidia ni kwamba wachezaji ninaocheza nao ni wale nilikuwa nakutana nao kama wapinzani, maisha yanaendelea ingawa kwa mabosi ndiyo igizo jipya nilikuwa chini ya wengine na sasa nipo yao ila wapo vizuri tu,"alisema.