#WC2018: Mfahamu Stanislav Cherchesov

Muktasari:

Cherchesov, alipewa kibarua cha kuinoa Russia mwaka 2016 na aliingoza timu hiyo katika mashindano ya kombe la mabara.

Huyu ni mlinda mlango wa zamani wa Umoja wa Kisovieti pamoja na Russia ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha taifa hili kilichoshiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 na 2002.

Cherchesov, alipewa kibarua cha kuinoa Russia mwaka 2016 na aliingoza timu hiyo katika mashindano ya kombe la mabara.

Kabla ya kupewa kibarua cha timu ya taifa, kocha huyu amewahi kuzifundisha klabu za Dynamo Moscow na Legia Warsaw.