Siri ya JPM kupewa jezi namba 19

UONGOZI wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, umeweka wazi siri ya kumkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, John Pombe Magufuli kuwa wamempa kama kumbukumbu ya wao kutwaa upingwa wa mara 19.
Simba wamemkabidhi kwa niaba Waziri Harrison Mwakyembe katika mkutano wa kupitisha katiba mpya uliofanyika jana katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kushindwa kufanya tukio hilo katika Uwanja wa Taifa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alisema wamefanya hivyo ili Rais abaki na kumbukumbu baada ya yeye mwenyewe kutukabidhi kombe la ubingwa wa 19 tangu timu yetu imeanzishwa.
"Tunaimani Rais wetu Magufuli ataipokea jezi hiyo na kubaki nayo kama kumbukumbu na tumempa na jezi nyingine ambayo imesainiwa na wachezaji wote pamoja na viongozi ambayo pia itakuwa kumbukumbu katika uongozi wake miaka yote," alisema.