Singida yachezea kipigo Copa Umisseta

Tuesday June 12 2018

 

By Imani Makongoro

Timu ya netiboli ya Mkoa wa Singida umechezea kipigo kizito cha magoli 64-19 dhidi ya Morogoro kwenye mashindano ya Copa Coca Cola Umisseta.
Singida buana imechezea kipigo hicho katika mchezo wa pili wa robo fainali ya netiboli leo Juni 12  kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba.
Wafungaji wa Singida, Asha Alfan na Hyfat Hassan walishindwa kufurukuta mbele ya walinzi wa Morogoro, Hadija Juma na Meryana Kizenga.
Kwenye mpira wa wavu, Dar es Salaam ilitembeza kipigo cha seti 3-0 dhidi ya Katavi huku kwenye kikapu Dar es Salaam tena iliwahenyesha Mtwara kwa pointi 103-15.