Singida United, Kakamega hapatoshi Kenya

Muktasari:

  • Singida iliondoshwa na Gor Mahia kwenye hatua ya nusu fainali wakati Kakamega Homeboys walitolewa na Simba.

Nakuru. Singida United watakuwa na barua kizito leo mchana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa mashindano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Kakamega Homeboys, leo Jumapili.


Singida iliondoshwa na Gor Mahia kwenye hatua ya nusu fainali wakati Kakamega Homeboys walitolewa na Simba.


Kocha wa Singida United, Hemed Morocco alisema baada ya lengo lao la ubingwa kutibuka, sasa wameweka nguvu kubwa kuhakikisha wanakuwa washindi wa tatu.


“Kakamega Homeboys ni timu ngumu. Imeifunga Yanga na imekwenda nan Simba hadi kwenye mikwaju ya penalti, itatupa wakati mgumu lakini nasi tuko vizuri,” alisema Morocco.