Simba yatinga uwanjani kwa miguu

Muktasari:

Kikosi hicho cha Simba kitashuka dimbani saa 10 jioni leo Alhamisi kupepetana na wenyeji Mabo FC ambayo imeapa kufa na Wekundu hao.

Mwanza. Simba imeingia uwanjani muda huu ikiwa na kikosi chake wakitokea mlango mdogo huku wakiwa kwa miguu bila gari lao.
Kikosi hicho cha Simba kitashuka dimbani saa 10 jioni leo Alhamisi kupepetana na wenyeji Mabo FC ambayo imeapa kufa na Wekundu hao.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongera alisema kikosi cha Simba kisitarajie kupata pointi kirahisi kutoka jijini hapo.