Simba yaikomalia Asante Kotoko Taifa

Timu ya Simba imetosa sare ya bao 1-1 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao la Simba liliwekwa wavuni na Emmanuel Okwi katika dakik ya 76 kipindi cha pili baada ya kutumia makosa ya mabeki wa Asante Kotoko.

Peter Salama alikosa penalti dakika za majeruhi baada ya kupiga shuti lililotua mikononi mwa kipa wa Asante Kotoko.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa dakika 44 na Micheal Yeboah kwa kichwa.

Bao ili lilikuwa shuti kali lililokwenda kugonga mtambao wa panya kisha Yeboah akamalizia na mpaka dakika 45 Simba wakaondoka mikono nyuma.

Simba walianza kwa kushambulia mashambulizi mara kwa mara ambayo hayakuweza kuzaa hata bao la kuotea.

Washambuliaji wa Simba Meddie Kagere na Emmanuel Okwi walitengenezewa nafasi nyingi za wazi lakini ngome ya ulinzi ya Asante Kotoko aliweza kuwazuia

Okwi ndani ya dakika 45 alitengenezewa nafasi tatu za kufunga ambazo mbili mabeki wa Asante Kotoko waliweza kuzuia na kuondoka hatari huku shuti lake lingine likitoka nje.

Kagere nae alikutana na nafasi mbili za kufunga shuti lake moja kali ndani ya boksi lilipanguliwa na kipa ikawa kona wakati nafasi nyingi uliokolewa na mabeki.

Simba mbili ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga walitawala mpira takribani kipindi chote cha kwanza ingawa walishindwa kufunga.

Nyota mpya wa Simba Cletus Chama ndio alikuwa kivutio na hatari zaidi kwa Asante Kotoko kwani ilionesha soka safi na kutengeneza nafasi za kufunga ambazo mastraika walishindwa kuzitumia.

Simba walilazima kufanya mabadiliko kipindi cha kwanza dakika 16 baada ya beki wa kulia Shomary Kapombe kuumia na nafasi yake aliingia Nicholas Gyan.

Kotoko wao walionekana kuamka zaidi dakika za mwisho kipindi cha kwanza kwani licha ya kufunga bao lakini walitengeneza pia nafasi ya kufunga ambayo kama si ubora wa Aishi Manula wangeweza kuandika bao la pili.