Sikia Mo Ibrahim anachosema

Wednesday July 12 2017

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. KIUNGO wa Simba, Ibrahim Mohamed, amesema ameitumia likizo yake kutathimini huduma yake kama ilikuwa na mchango katika kikosi chake na timu ya taifa, kisha akasaka mbinu mpya, maalum kwa msimu ujao.

"Simba ni klabu kubwa siwezi kucheza bila kujihoji kujua nilichokifanya kama kilikuwa na mantiki au la,kwani nina malengo yangu sichezi ili mladi," alisema

Kiungo huyo alisema amedhamiria kufanya kitu kipya msimu unaokuja, kitakachoonyesha ubora wa kazi zake kwamba zina mtazamo wa mbali.

"Kama mnavyojua Simba, imesajili kwa kasi nikimanisha kwamba ushindani utaanza kwetu wachezaji ambao utaleta manufaa kwenye timu,hilo linanifanya nijifue vya kutosha."