Saa 72 hatari ndani ya Yanga

Muktasari:

  • Zahera aliyerejea nchini akitokea kwao alikoenda kutekeleza majukumu ya timu ya taifa, DR Congo alisema kwa kuwa hakuwa na timu kwa muda atatumia siku zilizosalia kuwapika vijana wake kabla ya kuwavaa Chama la Wana. “Siwezi kukwambia programu yangu moja kwa moja nitaanzia wapi kwani sijakaa na timu, ila nimerudi na nataka kujua nyota wangu wana ufiti gani kabla ya kutumia sikui tatu kuwapika vilivyo,” alisema Zahera. Zahera alisema hatakuwa na muda wa kuwafundisha mbinu zaidi kuelekea mchezo huo kwani muda uliobaki ni mdogo sana atakachokiangalia ni kuwapa tizi la nguvu, kujiamini na kuhakikisha wanakuwa na pumzi za kutosha kabla ya mechi hiyo.

NYOTA wa Yanga wanapaswa kujipanga vilivyo, kwani Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera amesema atatumia siku tatu sawa na saa 72 kuwafua kabla ya kuwakabili Stand United katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Jumapili hii jijini Dar.

Zahera aliyerejea nchini akitokea kwao alikoenda kutekeleza majukumu ya timu ya taifa, DR Congo alisema kwa kuwa hakuwa na timu kwa muda atatumia siku zilizosalia kuwapika vijana wake kabla ya kuwavaa Chama la Wana. “Siwezi kukwambia programu yangu moja kwa moja nitaanzia wapi kwani sijakaa na timu, ila nimerudi na nataka kujua nyota wangu wana ufiti gani kabla ya kutumia sikui tatu kuwapika vilivyo,” alisema Zahera. Zahera alisema hatakuwa na muda wa kuwafundisha mbinu zaidi kuelekea mchezo huo kwani muda uliobaki ni mdogo sana atakachokiangalia ni kuwapa tizi la nguvu, kujiamini na kuhakikisha wanakuwa na pumzi za kutosha kabla ya mechi hiyo.

“Unajua wachezaji wanaweza kufanya vizuri kipindi cha kwanza ila wakachemsha kipindi, hiyo ni kuonyesha hawafanyi mazoezi mengi ya nguvu na kukimbia.”