Okwi tuliza mzuka

KOCHA Msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma, amesema hakuna mchezaji mwenye uhakika wa namba kikosini humo na wala hawaangalii jina la mtu.

“Tumefanya mabadiliko ili kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajacheza muda mrefu, katika mechi na Prisons wamecheza vizuri na kupata ushindi,” alisema.

“Mabadiliko yataendelea kufanyika zaidi katika mechi zijazo kutokana na kila mchezaji ambaye atakuwa anajituma bila ya kuangalia jila lake ni kubwa kwani tukifanya hivyo tutatengeneza usawa ndani ya timu na kila mchezaji kujituma zaidi.

“Tunatambua kuwa Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima ni wachezaji wazuri, lakini inatokea mechi nyingine wanabanwa au wanakuwa na matatizo binafsi ambayo yatawafanya kutokucheza vizuri, hapo tutawapa nafasi wengine kama ilivyokuwa kwenye mechi na Prisons, huo ndio msimamo wetu kikosini humu.”