Njombe Mji yazichokonoa Simba, Yanga

Wednesday September 13 2017

 

By GIFT MACHA

Licha ya kupoteza michezo miwili ya mwanzo wa msimu, Njombe Mji imepania kumaliza katika nafasi tatu za juu ambazo Simba, Yanga na Azam zimezoea kumaliza.

Mwenyekitu wa Njombe Mji, Erasto Mpete amedai kuwa licha ya changamoto wanazokutana nazo, bado malengo yao ni kumaliza nafasi za juu.

Mpete ambaye ni mjasiriamali anayejihusisha na biashara ya vyakula vya mifugo, amewahakikishia wapenzi wa timu hiyo kuwa mambo yatakuwa mazuri hivi karibuni.

"Malengo yetu ni kumaliza nafasi za juu, hasa ya kwanza mpaka ya tatu. Tukifeli kabisa basi tusikosekane kwenye 10 bora," amesema Mpete.

"Kuna changamoto kadhaa hasa katika gharama lakini tunajitahidi kwenda nazo sawa. Tunategemea sapoti kubwa sana ya wapenzi wa soka hapa Njombe," alieleza mwenyekiti huyo.