Neymar: Nimezaliwa upya ndani ya PSG

Muktasari:

  • Akiweka mbali kabisa na kusahau maisha Camp Nou, tayari Mbrazili huyo ameanza kujiona yuko nyumbani ndani ya Paris.

Baada ya kupata tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa kutegeneza mabao mawili na kufunga moja dhidi ya Guingamp, Neymar ameanza kufurahi maisha ndani ya Paris Saint-Germain, akisema ameanza maisha Ufaransa huku kukiwa na maneno mabaya kwa uamuzi wake wa kuondoka Barcelona.

Akiweka mbali kabisa na kusahau maisha Camp Nou, tayari Mbrazili huyo ameanza kujiona yuko nyumbani ndani ya Paris.

"Nimetulia hapa. Najua ilikuwa vigumu kwangu kuondoka Barcelona, lakini kwa sasa ninafuraha kuwa hapa," aliwaambia wanahabari baada ya mchezo huo.

"Watu walifikiri kuondoka kwangu Barcelona ndiyo mwisho wangu, lakini mambo yamekuwa ni tofauti na hapa najiona kama nimezaliwa upya.

"Ninafuraha na kuendelea kucheza soka kwa kiwango kile kile, kilichobadilika ni nchi, mji na timu.

"Jambo lililokuwa muhimu ni kushinda mechi zetu na timu kucheza vizuri ilikuwa ni mechi nzuri."

Katika mchezo huo wa kwanza wa Neymar alisaidia PSG kushinda mabao 3-0.