Mwili wa Masogange wafika nyumbani Mbeya

Muktasari:

Masogange atazikwa leo nyumbani kwao Mbeya

Mbeya. Mwili wa Marehemu Agnes Gerald 'Masogange' umewasili nyumbani kwao Utengule-Mbalizi,Mbeya saa 5:50.

Jeneza lililobeba mwili huo lilitolewa ndani ya gari hadi kuingizwa ndani umebebwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) 'Green Guard'.

Watu wanazimia baada ya kuona jeneza lenye mwili Masogange.

Wasanii wanashindwa kujizuia na kuangua vilio.

Wakati mwili wa marehemu ukiwa umebebwa kupelekwa ndani, wimbo wa msanii Bell 9 aliyomshiriki marehemu ndio umekuwa ukipigwa ikiwa ni ishara ya kuwafariji wafiwa, huku makundi tofauti tofuati ya vijana wameibuka na kuanza kucheza.