Mtaka apiga marufuku wanariadha kukimbia mbio za ndondo

Muktasari:

  • Mtaka amempongeza mwanaridha Ismail Juma iliyefanikiwa kuweka rekodi mpya ya taifa ya Tanzania  iliyokuwa ikishikiliwa na Dickson Marwa tangu mwaka 2008 baada ya kumaliza mbio hizo za km 21 kwa kutumia dakika 59:52 katika mbio zilizofanyika Jijini Mattoni, Jamhuri ya Czech.

.

Arusha. Rais wa Shirikisho la Riadha nchini (RT) Anthon Mtaka amewataka wanariadha kuacha kutumika katika mbio ndondo badala yake wajikite katika mbio za viwanjani kwa lengo la kusaka sifa za kushiriki mbio za Jumuiya ya Madola zinazotarajiwa kufanyika mwakani.

Mtaka amempongeza mwanaridha Ismail Juma iliyefanikiwa kuweka rekodi mpya ya taifa ya Tanzania  iliyokuwa ikishikiliwa na Dickson Marwa tangu mwaka 2008 baada ya kumaliza mbio hizo za km 21 kwa kutumia dakika 59:52 katika mbio zilizofanyika Jijini Mattoni, Jamhuri ya Czech.

“Mimi kama Rais na shirikisho kwa ujumla niwapongeze wanariadha ambao kwa mwaka huu wamekuwa nuru na mwanga katika kuhakikisha wanairudisha heshima ya mchezo huo nchini, lakini sasa wanatakiwa wajipange katika kufuzu nafasi ya kushiriki mbio za jumuiya ya madola mwakani."

Mtaka ametumia nafasi hiyo kuwataka wanariadha wote nchini kujitunza vizuri na kuacha kutumika katika mbio za barabarani badala yake wajipange vema katika mbio za viwanjani ili kupata nafasi ya kushiriki mbio za jumuiya ya madola mwakani kwani hilo ndio soko la riadha duniani.