Simon Msuva ateuliwa kikosi bora Morocco

Wednesday December 6 2017

 

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameteuliwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi bora cha mwezi uliopita kwenye Ligi Kuu ya nchini Morocco.
Msuva amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu ajiunge na klabu hiyo msimu huu akitokea timu ya Yanga ambayo aliiwezesha kuipa taji msimu uliopita.
Pia mchezaji huyo amejiweka kwenye nafasi nzuri katika timu ya Taifa kutokana na mchango wake kuonekana katika mechi mbalimbali alizocheza.