Azam yasajili kifaa kipya

KLABU ya Azam FC, imemsajili mshambuliaji, Benard Athur kutoka klabu ya Liberty Professionals  ya nchini Chana.

Azam inadaiwa kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili na amechukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wao, Mghana Yahya Mohamed aliyevunjiwa mkataba kwa makubaliano maalumu.

Hata hivyo, licha ya picha inayomwonyesha mchezaji huyo akikabiziwa jezi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam,  Abdul Mohamed, Afisa habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd Maganga hakutaka kuweka wazi na amesisitiza, taarifa kamili itatolewa kesho.

Huo ni usajili wa kwanza kwa Azam , waliofufanya katika dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15 na linatarajiwa kumalizika, Desemba 15.