Mikoa 11 kusaka ubingwa Taifa Cup

Muktasari:

Mashindano hayo ya netiboli ni sehemu ya kupata wachezaji wa kuunda kikosi cha timu ya taifa

Arusha: Mashindano ya Netiboli ya Taifa Cup inatarajia kuanza kutimua vumbi Jumatano mkoani Arusha kwa kushirikika timu za mikoa 11.

Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa netiboli mkoani hapa (chanea) Anna Mdoe alisema mikoa 11 ndio imedhibitisha ushiriki wa michuano hiyo msimu huu.

“Michuano hii ilikua ianze kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini Chaneta wakatuma taarifa kuwa wamepeleka mbele hadi kesho na hawakutueleza sababu za kufanya hivyo japo tunahisi sherehe za uhuru inaweza ikawa ni moja ya sababu” alisema Mdoe.

Mdoe alisema tayari maandalizi yamekamilika ikiwa pamoja na viwanja vya kuchezea na sehemu ya kufikia wachezaji na timu zinaanza kuwasili leo mkoani hapa.