UHONDO WA NOLLYWOOD: Mercy Aigbe akomaa na vipodozi

Muktasari:

Aigbe ambaye ni mama wa watoto wawili, ameanza kuuza vipodozi maalumu kwa ajili ya kuing’arisha na kuimarisha ngozi.

KATIKA kile kinachoonekana ni mkakati wa kujiongezea kipato zaidi ya kile anachokipata kwenye uigizaji, mwanadada Mercy Aigbe ameanzisha biashara ya vipodozi.

Aigbe ambaye ni mama wa watoto wawili, ameanza kuuza vipodozi maalumu kwa ajili ya kuing’arisha na kuimarisha ngozi.

“Watu wengi wananiuliza mbona rangi yangu inaonyesha mimi ni kijana na mrembo? Sasa nimeamua kuwapa majibu juu ya siri ya urembo wangu,” alisema Aigbe.

Mwanadada huyo amewaomba mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kumuunga mkono katika biashara yake.