Mbonde atimiza ndoto kuvaa medali Simba

Muktasari:

  • Ametaja sababu inayomfanya afurahie kuvaa medali hiyo kwamba itakuwa ya kwanza katika  ligi kuu ya VPL na ilikuwa ndoto yake kabla ya kutimkia kucheza soka la kulipwa nje.

BEKI wa Simba, Salim Mbonge amesema licha ya kutocheza mechi nyingi kutokana na kusumbuliwa na majeraha, anachoshukuru ni kwamba ni kati ya wachezaji ambao watavaa medali za ubingwa kwa msimu huu.

Ametaja sababu inayomfanya afurahie kuvaa medali hiyo kwamba itakuwa ya kwanza katika  ligi kuu ya VPL na ilikuwa ndoto yake kabla ya kutimkia kucheza soka la kulipwa nje.

"Tangu nianze kucheza ligi kuu sijawahi kuvaa medali, hili ni jambo la kihistoria kwangu, hata kwa badae ikitokea nihitaji kwenda kucheza nje, nadhani nitakuwa na cha kusimulia. "Nimepata medali nje ya ligi kuu ya VPL, Simba imenifanya ning'are licha ya kutocheza mechi nyingi kutokana na kuumia goti la mguu wa kulia  dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam," alisema.