Mbeya City, Alliance ni noma tupu leo

Muktasari:

  • Klabu hiyo imevuna pointi moja pekee dhidi ya African Lyon walipotoshana nguvu ya bao 1-1, huku Mbeya City wakiwa hawajapata pointi yoyote katika mechi tatu walizocheza na kufanya mtanange huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuwa mkali kwa pande zote.

ALLIANCE FC leo Jumapili inajitupa uwanjani kuivaa Mbeya City lakini Kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata ametamka hakuna kitu kingine walichokifuata mkoani humo zaidi ya kupata pointi tatu, ambazo zitawapa nguvu ya kupambana kwenye Ligi Kuu.

Klabu hiyo imevuna pointi moja pekee dhidi ya African Lyon walipotoshana nguvu ya bao 1-1, huku Mbeya City wakiwa hawajapata pointi yoyote katika mechi tatu walizocheza na kufanya mtanange huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuwa mkali kwa pande zote.

Makata alisema wanachohitaji kwenye mchezo ni ushindi kwa namna yoyote ili kujinyakulia alama tatu na sio vinginevyo.

Aliongeza kwa muda waliokaa mapumziko wamejiandaa vya kutosha na wachezaji wote wana ari nzuri na nia yao ni kucheza kwa umakini kuhakikisha hawapotezi mechi hiyo.

“Tutapambana kadri ya uwezo wetu na malengo ni kushinda hatutaki sare wala kupoteza, tumejipanga vizuri na muda ambao ligi imesimama tulifanya maandalizi ya ziada, hivyo tunaingia uwanjani kwa nguvu zote, ” alisema Makata.

Nahodha wa Klabu hiyo, Hans Masoud alisema hawatakuwa tayari kupoteza mchezo huo na watacheza kwa tahadhari kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea tangu mwanzo wa msuimu wa ligi.