Mastaa Simba wapewa mchongo

Muktasari:

  • Mchongo huo umetolewa na nyota wa zamani wa klabu hiyo akiwamo beki, Boniface Pawasa na Ulimboka Mwakingwe waliosema kama mastaa wa timu hiyo hawatakuwa na malengo nje ya viongozi wao, itakuwa vigumu kufanya kweli.

Dar es Salaam.Nyota wa Simba wamepewa mchongo ili waweze kuwakuna mashabiki wa klabu hiyo kwa kutakiwa kucheza kwa malengo na ikiwezekana kutetea taji lao la Ligi Kuu Bara.

Mchongo huo umetolewa na nyota wa zamani wa klabu hiyo akiwamo beki, Boniface Pawasa na Ulimboka Mwakingwe waliosema kama mastaa wa timu hiyo hawatakuwa na malengo nje ya viongozi wao, itakuwa vigumu kufanya kweli.

Nyota hao wa zamani walitoa maoni hayo baada ya kushuhudia Simba ikishindwa kuwakuna mashabiki kwenye Simba Day walipotoka sare ya 1-1 na Asante Kotoko ya Ghana.

"Kilichoonekana Simba Day ni viongozi kufanya kazi yao kikamilifu, lakini wachezaji kwa upande wao walifanya kwa ulegevu, ingawa zilikuwepo juhudi za mtu mmoja mmoja, sasa wanapaswa kujiwekea malengo wanapokaa kambini kuhamasishana juu ya ubingwa wa ligi inayotarajia kuanza Agosti 22," alisema Pawasa,

Naye ulimboka alisema kwa miaka kadha ya nyuma viongozi ndio walionekana tatizo kwa kusajili wachezaji ambao hawakuwa na hadhi ya kuvaa uzi mwekundu, lakini kwa sasa wamefanikiwa kulirekebisha hilo msala utabakia kwa wachezaji tu.