Chopa aachiwa siri nzito na Masogange

Muktasari:

Chopa aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha wasanii kuhusu maandalizi ya mazishi ya Masogange yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya Jumatatu.

Dar es Salaam. Msanii Juma Chikoka 'Chopa', swahiba wa karibu wa Agnes Masogange amesema marehemu dakika chacha kabla hajafariki, amemwambia mambo mawili makubwa aliyotaka watanzania wayajua atayasema kesho Jumapili wakati wa kuuaga mwili wake kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.

Chopa aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha wasanii kuhusu maandalizi ya mazishi ya Masogange yanayotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya Jumatatu.

 Chopa aliyeshuhudia dakika za mwisho za kupigania uhai wake za Masogange alisema mrembo huyo amemuachia ujumbe mzito aliotaka Watanzania wajue.