Mashabiki wa Everton Dar es Salaam watinga jezi mpya za Everton msimu 2017/18

Muktasari:

Jezi hizo mpya zilizotangazwa siku chache zilizopita watakayotumia Everton ugenini msimu wa 2017/18.

Dar es Salaam. Mashabiki waliojitokeza kuwalaki wachezaji wa Everton jijini Dar es Salaam jana wamegawiwa jezi mpya za timu hiyo ambapo wao  wamekuwa mashabiki wa  kwanza kuzivaa tangu zitangaze siku tatu zilizopita.

Jezi hizo mpya zilizotangazwa siku chache zilizopita watakayotumia Everton ugenini msimu wa 2017/18.

Msimu ujao Everton watavaa jezi za rangi ya kijivu watakapokuwa wakicheza ugenini.