Manara aifafananisha Simba na Bayern Munich

Wednesday May 16 2018

 

Dar es Salaam. Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kwamba klabu yao anaifananisha na Bayern Munich ya Ujerumani na kusema klabu zingine zitaendelea kufukuzana nafasi ya pili na tatu.

Manara alisema Simba imekuwa ni klabu pekee inayofanya vyema na yenye historia ya kipekee kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa ubora.

Manara alionya kuwa klabu hiyo ni mali ya watu wopte hasa mashabiki na siyo mali ya mtu mmoja. Hivyo akawataka mashabiki hao kujiandaa kuhudhria mkutano mkuu ambao unatarajiwa kufanyika kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuanza.