Mama amtabiria Hamisa kuzaa pacha

Monday April 16 2018

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mwanamitindo, Hamisa Mobeto anatarajiwa kuzaa watoto mapacha kama ataamua kuzaa tena hapo baadaye.

Hayo yamebainishwa na Mama yake Shufaa Rutiginga, alipozungumza na MCL Digital, alidai kwamba katika familia yao kuna mapacha hivyo ana imani mtoto wake akiendelea kuzaa naye atakuja kupata mapacha.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa tayari ana watoto wawili Fantisy na Dyllan aliyezaa na msanii Naseeb Abdul’Diamond’, mama yake anamuombea azae watoto sita na kati ya hao anaamini atazaa mapacha.

Kuhusu kuzaa na wanaume tofauti, mama huyo alisema haoni shida, na yupo tayari kuendelea kuletewa wajukuu bila kujali mtoto wake huyo atazaa nani.

“Unajua Hamisa nimemzaa peke yake, hivyo naamini watoto ndio watakuwa ndugu zake na wataweza kumsaidia ikiwa kesho  na keshokutwa nikiwa sipo duniani.

“Kila siku ninaomba idadi hiyo ya wajukuu  ifike nikiwa na nguvu zangu niwashuhudie na kushiriki katika kuwalea kama bibi ,”amesema Shufaa.

Akizungumzia kuhusu baba wa wajukuu zake, mama Mobeto amesema ni baba bora wote wanawatunza watoto wao na kuongeza kuwa anawapenda.