Mahrez yuko sokoni kwa bei poa

LEICESTER, ENGLAND. LEICESTER City amekubali kushusha bei ya kiungo wa Riyad Mahrez hadi kufikia Pauni 40 milioni jambo linalozifanya Arsenal na Tottenham kuanza kutoana macho kuitaka saini yake.

Mahrez anajiandaa kuachana na Leicester City baada ya kushinda taji la Championship na Ligi Kuu England kwa miaka mitatu aliyodumu kwenye klabu hiyo.

Mahrez, 26, ambaye alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2016 baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba ubingwa na baadaye akasaini mkataba mpya wa miaka minne.

Lakini, Mahrez hana mpango wa kuendelea kubaki kwenye timu kwa miaka yake yote ya mkataba na hivyo kufungua njia kwa timu zinazohitaaji saini yake.