Mabeki waipa Lyon hasira ya usajili wapya

Sunday November 12 2017

 

By Charles Abel

KIPIGO cha mabao 3-0 kutoka kwa Mshikamano FC kimeifanya African Lyon iingie kwa fujo kwenye dirisha dogo la usajili ambapo italazimika kufanya mabadiliko makubwa hasa kwenye safu yake ya ulinzi.

Lyon licha ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi A ikiwa na pointing 17, ni moja imekuwa ni moja ya timu zenye safu dhaifu ya ulinzi katika kundi hilo ikiwa imefungwa mabao tisa katika mechi tisa ilizocheza hadi sasa ikiwa ni wastani wa bao  moja kila mechi.

"Ni kweli ni lazima tufanye usajili hasa unaohusu wachezaji wazoefu ambao watatusaidia katika hizi mechi zilizobakia ili tuweze kutimiza malengo yetu ya kupanda Ligi Kuu.

Usajili wetu utahusu idara karibia zote za timu ambao ni kuanzia kwenye safu ya ushambuliaji, kiungo na beki ambazo zote zimeonyesha kuhitaji watu wenye uzoefu wa hali ya juu kuliko hawa waliopo," alisema kocha wa Lyon Renatus Bernard.

Ukiondoa safu ya ulinzi, Lyon pia inapaswa kuongeza makali yake kwenye safu ya ushambuliaji ambayo bado imekuwa ikisuasua kwa kupoteza idadi kubwa ya mabao katika mechi walizocheza.